Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, anawakumbusha wafanyabiashara wote kuhuisha leseni zao za biashara kwa wakati ili kuepuka adhabu zinazotokana na kuchelewesha kuhuisha leseni. Mfanyabiashara upewa siku 21 kuhuisha leseni yake pindi inapokwisha muda wake bila adhabu yoyote lakini akichelewa kuhuisha leseni ndani ya siku hizo 21 hupewa adhabu ya asilimia 25 ya kiwango cha leseni yake.Hivyo, mnakumbushwa kuihuisha ili kuepuka adhabu kwa waliopo ndani ya siku 21 tangu leseni ilipomaliza muda wake na kwa wale ambao wapo zaidi ya siku 21 wataepuka kuendelea kuongezeka kwa kiwango cha adhabu. Huisha leseni yako popote ulipo kupitia mfumo wa tausi kwa kiunganishi tausi.tamisemi.go.tz
Lipa kodi kwa maendeleo ya Halmashauri yako.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa