Na:John A.Mganga( I.O Nsimbo DC )
Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wametakiwa kujidhatiti katika kudhibiti mapato ya Halmashauri ili kuondoa uwezekano wa kupoteza mapato katika maeneo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Madiwani Aprili 20 2017 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo na Diwani wa Kata ya Machimboni Mh.Raphael Kalinga amesema jitihada za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa mapato ya Halmashauri yanadhibitiwa ipasavyo jambo litakalosaidia kuboresha mapato na kuondokana na tatizo la uhaba wa fedha unaochelewesha kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenyekiti amewataka watendaji wa Halmashauri Nsimbo kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato vitakavyowezesha Halmashauri kuongeza mapato jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya Halmashauri ya kuwaletea wananchi Maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo pia ametumia nafasi hiyo kuwataka watendaji wa Kata na Vijiiji kuwajibika ipasavyo kwa nafasi zao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Taarifa za Utekelezaji za Kata zinaandaliwa na kufikishwa katika Vikao vya Baraza la Madiwani mapema jambo litakalosaidia kujadili kwa wakati Taarifa hizo huku akisisitiza kutosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa Madiwani ambao watashindwa kufikisha Taarifa za Utekelezaji wa Kata zao kikaoni.
Mwenyekiti huyo katika kutilia mkazo kile anachozungumza na anachokisimamia ametoa adhabu kwa kuwatoa nje Diwani wa Kata ya Kapalala Mh.Reward Sichone pamoja na Diwani wa Kata ya Katumba Seneta Baraka Jetty, kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa wakati Taarifa za Utekelezaji za Kata zao Kikaoni ambapo madiwani hao waliheshimu maamuzi ya Mwenyekiti wao na kukubali adhabu iliyotolewa.
Kalinga amekemea vikali tabia ya kutokuwasilisha Taarifa za Vikao kwa wakati na kuwataka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo pamoja na Afisa Utumishi kufuatilia kwa karibu kubaini chanzo cha tatizo hilo na kwamba hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wanaokwamisha Uandaaji wa Taarifa kwa Wakati.
Kalinga pia amewataka madiwani kushirikiana kwa karibu sambamba na kuboresha mahusiano mema na Wataalamu wa Halmashauri katika kata zao jambo litakaloboresha utendaji kazi wenye kuleta tija kwa Halmashauri kiujumla.
Mkutano wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo umefunguliwa leo kwa Madiwani kuwasilisha Taarifa mbalimbali za Utekelezaji za Kata ambapo kikao hicho kitamalizika Aprili 21 mwaka 2017.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +255785659744
Simu: +25585659744
Barua pepe: info@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa