Nsimbo- Kapalala
Mbegu ya ufuta Tani 2.24 inatarajiwa kusambazwa kwa wakulima wa zao la ufuta katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ikiwa ni jitihada za Halmashauri ikishirikiana na Serikali Mkoani Katavi kuboresha Kilimo cha zao hilo la kimkakati.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Bw. Paul Sheyo amesema tayari mbegu hiyo ya ufuta tayari imepokelewa kutoka kwa wakala wa mbegu Nchini ASA na inatarajiwa kugawanywa katika vyama Vinne vya Ushirika vya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ili wakulima katika vyama hivyo vya Ushirika waweze kugawiwa kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya kilimo cha zao hilo.
Bw.Sheyo amesema mbegu hiyo bora ya Ufuta itakayotolewa itatosheleza Ekari 1122 za wakulima wa zao hilo la kimkakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo wakulima wengine wanaolima zao la Ufuta ambao hawatabahatika kufikiwa na mgao wa mbegu bora ya ufuta wameshauriwa kununua mbegu bora ya ufuta kwa wasambazaji wa pembejeo za kilimo.
Amewaasa wakulima wa mazao ya Biashara Nsimbo kuhakikisha kuwa wanashirikiana kwa karibu na wataalamu wa Kilimo katika ngazi ya Vijiji na Kata ili waweze kupata elimu itakayowawezesha kutumia mbinu bora na za kisasa akatika kilimo cha mazao hayo ya Kibiashara ili kuongeza tija katika Uzalalishaji
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa