Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wametakiwa kutumia vema msimu wa Mvua zilizoanza kunyesha hivi karibuni kupanda miti ya kutosha ili kufikia malengo mahsusi ya Halmashauri ya kupanda miti kwa wingi zaidi ili kuifanya Nsimbo kuwa ya Kijani.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Nsimbo Bw.Mugeta Masambu ameeleza kuwa hatua ya Wananchi kupanda miche ya miti kwa wingi kipindi cha mvua itasaidia kwa kiasi kikubwa miche hiyo kustawi kwa haraka kutokana na uwepo wa maji ya kutosha kipindi hiki cha Msika.
Ameongeza kuwa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Nsimbo imekuwa ikihamasisha Wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuhakikisha kuwa matakwa ya Kisera ya Serikali yanatekelezwa kikamilifu ili malengo mahsusi ya Serikali ya kutunza mazingira yanatimia.
Mbali na upandaji wa Miti Wananchi Nsimbo pia wametakiwa kuhakikisha kuwa wanafyeka nyasi na vichaka mara kwa mara katika msimu huu wa mvua kwa kuwa nyasi kipindi cha mvua huzaliana kwa wingi na kuwa chanzo cha mazalia ya mbu wasababishao malaria.
Hivyo ili kupunguza kuenea kwa malaria Wananchi wameshauriwa kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ambayo yanaweza kutuamisha maji katika kipindi hiki cha mvua ili kudhibiti mazalia ya mbu jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa malaria Nsimbo
Wananchi pia wametakiwa kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa safi kwa kuhakikisha kuwa wanajenga mazoea ya kutotupa takataka hovyo pamoja na kuepuka kutiririsha maji taka kipindi hiki cha masika ili kudhiti kuenea kwa magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa