Pichani:Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akimkabhi cheti cha Ushindi wa Nafasi ya Ubunge Mgombea Ubunge jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe mara baada ya kutangazwa mshsindi katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu ngazi ya Ubunge leo 29,Oktoba 2020.
Nsimbo-Isinde
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani amemtangaza Mgombea Ubunge jimbo la Nsimbo kupitia tiketi ya CCM Ndugu Anna Richard Lupembe kuwa Mh.Mbunge wa Jimbo la Nsimbo.
Hatua ya kumtangaza Mshindi wa kinyang’anyiro cha nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nsimbo inakamilika majira ya saa mbili asubuhi ya Tarehe 29 Oktoba 2020 baada ya matokeo kutoka katika kata zote 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kuwasilishwa katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nsimbo na kukamilika kwa taratibu zote za Tume ya taifa ya Uchaguzi.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa Nafasi ya Ubunge Jimbo la Nsimbo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Bw.Mohamed Ramdhani amesema Ndugu Anna Richard Lupembe,Mgombea Ubunge Jimbo la Nsimbo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM amekuwa Mshindi wa Kiti cha Ubunge Jimboni Nsimbo baada ya kufanikiwa kujipatia kura 38,346 dhidi ya Wapinzani wake.
Msimamizi wa Uchaguzi Nsimbo amevitaja vyama Vingine vya Siasa viliyoshiriki katika Kinyang’anyiro cha Nafasi ya Ubunge kuwa ni pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Chama cha ACT Wazalendo,CHAUMA na Chama cha Mapinduzi CCM .
Amewataja wagombea wa Vyama vingine vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi kuwa ni pamoja na Omar Faraji ambae amepata kura 904,John Malak kutoka chama cha ACT Wazalendo ambae amepata kura 1292,Gdfrey John Nkasu wa Chama cha Chauma ambae amepata kura 1159.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa