Pichani:Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi Kajoro Vyohoroka akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo iliyofanyika leo Machi 29 kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu Kanuni za Kudumu za Halmashauri(Picha na John Mganga)
Madiwani kutoka Kata 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo leo Machi 29 2018 wamepatiwa Semina ya siku moja ya kuwajengea uelewa wa Kanuni za Kudumu za Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mwailwa Smith Pangani amesema Semina hiyo ya siku moja imeandaliwa kwa lengo la kuwajengea uelewa Madiwani kuhusu Kanuni za Kudumu za Halmashauri ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya usimamizi wa shughuli mbalimbali katika kata zao kwa kuzingatia Kanuni Sheria na Taratibu za Halmashauri.
Akifungua Semina hiyo ya siku moja ,Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi Kajoro Vyohoroka amesema Mafunzo ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri yatawasaidia madiwani kuwa na uelewa wa kutosha na hivyo kushirikiana kwa karibu na Wataalamu wa Halmashauri yao katika kutekeleza shughuli mbalimbali za Kimaendeleo.
Amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwani yatasaidia madiwani hao kuwa na uelewa kuhusu taratibu za uendeshaji wa vikao mbalimbali vya Halmashauri jambo litakalowasaidia Madiwani hao kufuata utaratibu.
Amesema ni jukumu la Madiwani kuhakikisha kuwa wanajenga mahusiano mema baina yao pamoja na kushirikiana kwa karibu na Wataalamu wa Halmashauri ambapo kufanya hivyo kutasaidia kwa sehemu kubwa kutekeleza kwa ufanisi shughuli mbalimbali za maendeleo na hivyo kufikia lengo la Serikali la kuboresha huduma za jamii kwa Wananchi
Bw.Kajoro pia amesisitiza kuwepo na utaratibu wa kutoa mrejesho kwa wananchi kwa kutumia njia mbalimbali za kuwafikia wananchi zikiwemo mbao za matangazo katika Ofisi za Kata ama katika mikutano yao ya hadhara jambo litakalosaidia wananchi kujenga imani na serikali
Ameongeza kuwa ni vema madiwani wa Halmashauri wakawa na kauli moja badala ya kutofautiana kimtazamo pindi wanapotoka nje jambo linalowachanganya wananchi na hivyo kuwafanya wananchi kutokuwa na Imani na Viongozi waliowachagua
Pamoja na mambo mengine amewataka madiwani na wataalamu kutambua kuwa mahusiano kati ya chama na Serikali ni muhimu kwa kuwa wataalamu wanatekeleza Ilani ya chama kilichopo madarkani hivyo ni muhimu kuboresha mahusiano mema na chama kilichopo madarakani kufikia lengo la utoaji huduma bora kwa wananchi
Amesema ikiwa madiwani watakuwa na mahusiano mema na wataalamu itasidia kwa sehemu kubwa madiwani kueleweshwa na kupewa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayowatatiza jambo litakalowasaidia kuleta tija katika utendaij kazi.
Kwa upande wao madiwani waliopatiwa mafunzo hayo wameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kuandaa semina hiyo ambapo wamesisitiza mafunz hayo kuwa endelevu ili kuwajengea uelewa zaidi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +255785659744
Simu: +25585659744
Barua pepe: info@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa