Nsimbo -Katumba
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni miongoni mwa Halmashauri 3 za Mkoa wa Katavi na Halmashauri 11 za Mikoa ya Nyanda za juu kusini zinazotarajia kunufaika na Mradi wa Kilimo bora cha Mboga mboga na matunda kwa Wanawake na Vijana KIBOWAVI.
Mratibu Mradi wa KOBIWAVI Mkoa wa Katavi Bw.Christopher Chaula ameeleza kuwa lengo kuu la Mradi huo wa Shirika la HELVETAS Tanzania utakaotekelezwa kwa miaka minne kuanzia Februari 2020 hadi Februari 2024 kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya, ni kuchangia katika ukuaji wa uchumi jumuishi, kuendeleza sekta binafsi na kuzalisha ajira katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mbogamboga na matunda pamoja na kuongeza usalama wa chakula na Lishe katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Katumba eneo la Mnyaki Sokoni katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani 16 Oktoba 2020 Chaula ameeleza kuwa utekelezaji wa Mradi huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo unatarajia kuanza rasmi mapema 2021 ambapo utatekelezwa katika Kata 7 za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo vikundi 100 vya Ujasiriamali vya Wanawake na Vijana vinatrajia kunufaika na Mradi huo.
Chaula amesema,Mradi wa KIBOWAVI kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo unatarajia kutekeleza shughuli zake za kuchagiza kilimo cha mbogamboga na matunda katika Kata 7 ambapo utekelezaji wake utaanza kutekelezwa kupitia Vikundi vya Wanawake na Vijana vya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo vinavyojihusisha na Kilimo cha Mboga mboga na matunda.
Ameeleza kuwa Mradi huo utaanzisha mashamba darasa ya Kilimo cha Mbogamboga na matunda ili kutoa elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya Mbogamboga na matunda Nsimbo lengo kuu likiwa ni kuchangia katika ukuaji wa uchumi jumuishi na kuzalisha ajira katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mbogamboga na matunda.
Aidha Chaula amesema Elimu juu ya mbinu bora za Kilimo cha mbogamboga na matunda itatolewa kwa wakulima Viongozi wa mazao ya mbogamboga na matunda Nsimbo ambapo kupitia Wakulima Viongozi hao wazalishaji watapata elimu ya namna ya kulima mazao ya matunda na mbogamboga.
Chaula pia ameeleza kuwa KIBOWAVI imedhamiria kujenga uwezo kwa wazalishaji wa matunda na mbogamboga ili waweze kuweka na kukopa kupitia vikundi vyao vya uzalishaji wa mazao ya matunda na mbogamboga.
Mradi wa Kilimo bora cha Mbogamboga na matunda kwa Wanawake na Vijana KIBOWAVI ni moja kati ya Miradi inayotekelezwa na Shirika la HELVETAS Tanzania Nchini ukifadhiliwa na Umoja wa Ulaya kwa silimia 90 ambapo Asilimia 10 unafadhiliwa na Mshirika kiongozi HELVETAS Tanzania ambapo washirika wengine wa KIBOWAVI ni Shirika la CODERT,ADP Mbozi,na TAFOPA.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa